Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amesema mashamba yote yanayofutwa wapewe wananchi bure, ni mali yao. Walidhulumiwa kipindi cha miaka ya nyuma na wakubwa fulani kujimilikisha.

Aidha, Rais John Magufuli ameagiza wafanyabiashara ndogondogo wa Stendi ya Morogoro kutobugudhiwa, amchaia Shilingi laki moja mama aliyeibua kero hiyo

Amewataka Watanzania kubadilika kwa kuwekeza katika viwanda, kwamba suala la viwanda linawezekana nchini

Rais amesema “Tusirudie tena kuua viwanda Serikali nitaunga mkono viwanda vyote vinavyoanzishwa. Nafahamu kuna baadhi ya vikodi kodi vinavyoleta kero, tayari nimeshatoa maelekezo kwa waziri wa viwanda kuangalia upya hizo kodi,”.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *