Muigizaji wa Bongo Movie, Irene Uwoya amemchimba mkwara mume wake ambaye pia ni msanii wa bongo fleva Dogo Janja, iwapo atafanya jambo na wanawake wengi huwa hawalipendi.
Kwenye ukurasa wake wa instagram, Irene uwoya amepost picha ya dogo ikiwa na caption kuwa msanii huyo huenda akaoa mke wa pili, na kuandika ujumbe ambao unaonyesha hakutakuwa na amani baina ya waili hao.
Ameanza kwa kuandika “Ndo utajua mimi Kabila gani…thubutu uwone tena wasikudanganye Dogo Janja”, ameandika Irene Uwoya.
Baada ya mkwara huo watu walionesha kmshangaa Uwoya kwa uamuzi huo, wakisema kwamba hakupaswa kusema hivyo kwani dini inamruhusu Dogo Janja kufanya hivyo.
Siku chache zilizopita Dogo Janja alisema kuwa anaweza kuoa mke wa pili kwa kuwa dini yake inaruhusu kufanya hivyo.