Naibu Waziri Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa, na Michezo, Juliana Shonza amesema sheria hairuhusu wimbo uliofungiwa nchini kutumika katika show nje ya nchi.
Naibu Waziri amesema hayo jana ambacho kuliwakutanisha wasanii, wizara na Baraza la Sanaa Taifa (BASATA).
Amesema “Sheria hairuhusu wimbo wa msanii husika uliofungiwa hapa Tanzania kwenda kuufanyia show nje ya nchi. Endapo atafanya hivyo atakuwa anakiuka kanuni na sheria za nchi.” amesema Juliana Shonza.
February 28 mwaka huu Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ilipokea list ya nyimbo 15 zisizokuwa na maadili kutoka kwa Baraza la Sanaa Taifa (BASATA) na kuamuru kutopigwa katika vyombo vya habari.