Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Aslay, amefunguka kuhusu kumpiga marufuku mama mtoto wake, kufanya kazi aliyokuwa akiifanya.

Aslay amesema mama mtoto wake ambaye anafahamika kwa jina la Tessy, hawezi akaendelea kufanya kazi ya aliyokuwa akifanya ya ‘video vixen’, kwani amempiga marufu na kila alichokuwa akitafuta anampatia.

Amesema kuwa “Hawezi kuendelea mimi ndio nimesema hawezi kuendelea, sidhani kama sasa hivi anapenda tena kufanya, kwa sababu mara nyingi yupo na mtoto, na yeye  mwenyewe kuna mambo yake anafanya kitu kinachomuingizia hela, kwa sababu kule alikuwa anatafuta hela sasa hivi hela anapata”,.

Msanii huyo pia ameweka wazi kuhusu tetesi za kuachana na mama mtoto wake huyo, na kusema kwamba hajawahi kuachana wala kutengana naye.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *