Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Riyama Ally amesema moja ya tabia zinazomchanganya kutoka kwa mume wake, Leo Mysterio ni kupewa mabusu ya kila mara.
Muigizaji huyo amesema kuwa kitendo hiko kimekuwa kama mfumo wa maisha yao kwasasa.
Amesema kuwa Naona kama ananiibia mabusu yale, ana mabusu huyu kulamba lambana kama majibwa.
Pia ameongeza kwa kusema Nikirudi tu huko kwenye mapunziko mimi nakula mabusu, nachodolewa chondole tena kama mtoto wa njiwa, unajua tena mzaramo na mibusu.
Kwa upande mwingine Riyama amesema kuwa suala la kuongeza mtoto katika familia yao ni mipango ya Mwenyenzi Mungu hivyo wanavuta subra.