Mwanamuziki wa dansi nchini, Papii Kocha amefunguka na kuweka wazi masuala mbalimbali kuhusu maisha yake ya jela.
Papii Kocha amesema kuwa wakati alipokuwa Gerezani alikuwa kwenye kitengo cha washonaji kofia na kwasasa anajua vizuri kushona baada ya kujifunza akiwa gereza la Ukonga jijini Dar es Salaam.
Pia Papii Kocha amesema kuwa wakati anahukumiwa kwenda jela aliacha mwanamke na mtoto wa miaka 4 lakini saivi katoka kamkuta ana miaka 18 na mwanamke wake aliyemuacha kakuta yupo na mtu mwingine.
Mwanamuziki huyo ameongeza kwa kusema kuwa hawezi kumlaumu mwanamke huyo kwasababu kifungo chake kilikuwa kikubwa sana na mwanamke hawezi kukusuburia mpaka utoke.
Kwa upande mwingine mwanamuziki huyo amewataka mashabiki wake kufika kwa wingi katika show yao itakayofanyika katika ukumbi wa Kings Solomoni Namanga jijini Dar es Salaam.