Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz ameweka wazi mipango yake ya ndoa huku akiomba baraka kutoka kwa mama yake mzazi.

Kupitia akaunti yake ya Instagram Diamond amemtakia mama yake heri ya siku ya wanawake ambapo amemshukuru kwa malezi aliyompa tangu akiwa mtoto mdogo hadi kuwa na mafanikio makubwa.

Ameanza kwa kuandika “Happy Women’s day Mama na wanawake wote Ulimwenguni… Nashkuru sana kwa kunizaa na kunilea…Wewe ni Mboni na Nguzo ya Maisha yangu mama…Licha ya shida na Mateso uliyoyapata kwenye kunizaa na kunilea, lakini hata sasa ambapo ulitakiwa walau Upumzike nimekuwa nikikukosea kwa kukuingiza hata kwenye Matatizo Yasiyokuhusu…Wanakutukana, wanakukebehi na kukutupia kila neno lililo baya, yote kwa sababu yangu mimi, lakini sikuzote umekuwa mwenye kunisamehe, kunipenda na Kunithamini.

Pia ameandika Nakupenda sana Mama, Na nisameh kwa yote nilokukosea… Inshaalah, Mwenyez Mungu anibariki Mwaka huu Mwanao nifanikishe Ndoa yangu na kukupa Furaha ya Milele ambayo siku zote umekuwa Ukiitaka….. @mama_dangote.

Lakini Diamond hajaweka wazi ni mwanamke gani atakayefunga nae ndoa kutokana na kuachana na mzazi mwenzake, Zari The Boss Lady.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *