Mbunge wa Jimbo la Hanang, mkoani Manyara, Dkt Mary Nagu (CCM) na mwenyekiti wa CCM wilaya hiyo waanashikiliwa na Jeshi la Polisi wilayani humo.

Amri ya kukamatwa kwa mbunge huyo imetolewa na Mkuu wa wilaya hiyo kutokana na sababu ya  kushindwa kuelewana kiutendaji.

Kwa mujibu wa mkuu wa wilaya Sarah Msafiri ameeleza kuwa ameagiza kukamatwa kwa Mbunge huyo baada ya kuchoka kumvumilia kutokana na kauli anazozitoa kwenye mikutano yake na wananchi akihamasisha wasishiriki shughuli za maendeleo.

Pia amemtuhumu Mbunge huyo kuwataka wananchi wasishirikiane naye jambo ambalo alidai ni sawa na kuwataka wananchi wasishirikiane na serikali kwa sababu yeye anasimama kama serikali.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *