Mwanamuziki wa dansi nchini, Papii Kocha amesema kuwa anaona fahari na ushujaa kila anapomuangalia mtoto wake Asha ambaye alimuacha akiwa mdogo wakati akitumikia kifungo.

 

Papii amesema kuwa alipokuwa gerezani takriban miaka 14, hakupata muda mzuri wa kukaa na mtoto wake huyo zaidi ya alivyokuwa akienda kumsalimia gerezani.

 

Mwanamuziki huyo amesema kuwa kwasasa ameona afanye kila analoweza mwanaye aweze kufaidi angalau matunda na furaha aliyoikosa kwa muda mrefu kutoka kwake.

 

 

Kwa upande mwingine Papii amewaomba mashabiki wake wajitokeze kwa wingi kwenye shoo yao inayotarajiwa kufanyika Machi 10, mwaka huu katika Ukumbi wa King Solomon.

 

Papii Kocha aliachiliwa huru kutoka gerezani kwa msamaha wa rais Magufuli baada ya kukaa jela kwa miaka 14.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *