Serikali ya Tanzania kupitia kwa wizara ya habari, utamaduni sanaa na michezo imelifungia gazeti la kila wiki la MSETO kwa tuhuma za kuchapisha habari za uongo.

Waziri wa wizara ya habari, utamaduni, sanaa na michezo, Nape Nnauye ametangaza kulifungia gazeti hilo kwa kipindi cha miaka mitatu (miezi 36) kuanzia tarehe 11 Agosti 2016.

Waziri Nape amelishutumu gazeti hilo kwa uandishi usiozingatia weledi na miiko ya taaluma hiyo.

mseto

Nape amesema kuwa gazeti hilo limekuwa likitumia nyaraka bandia za serikali kitu ambacho kinaharibu sura ya rais John Magufuli na watendaji wengine wa serikali.

Gazeti hilo lililokuwa likichapishwa kwa njia ya karatasi, kwa sasa limezuiwa kutoa machapisho kwa njia yoyote ile ikiwemo njia ya kielektroniki.

 

 

 

 

 

 

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *