Moto mkubwa umelipuka na kuunguza soko la wafanyabiashara wadogo wadogo katika eneo la Mbagala Rangi Tatu – Dar es Salaam.
Sehemu iliyoathirika zaidi ni ile ya wauza mitumba huku baadhi ya bidhaa zao zikiteketea kwa moto lakini hakuna aliyeripotiwa kupoteza maisha wala kujeruhiwa.
Chanzo cha moto huo kinadhaniwa kuwa ni hitilafu ya umeme ambapo tayari gari la jeshi la zima moto limefika kuzima moto huo.
Moto huo umetokea leo mida ya asubuhi ambao inasemekana ulisababishwa na itilafu ya umeme mpaka kupelekea kuungua kwa soko hilo.