Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe ameruhusiwa kutoka hospitali baada ya madaktari kujiridhisha kuwa afya yake imeimarika.

Mbowe alilazwa hospitali ya KCMC mkoani Kilimanjaro kuanzia juzi usiku ambapo alikuwa akisumbuliwa na maumivu makali ya kichwa.

Afisa Habari wa KCMC, Gabriel Chisseo amesema kuwa Mbowe ameruhusiwa kutoka hospitalini hapo, baada ya madaktari waliokuwa wakimpatia matibabu kuona afya yake inazidi kuimarika.

Mbowe alifikishwa KCMC Machi 4 akiumwa kichwa, na jana Machi tano aliruhusiwa kutoka hospitalini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *