Mchekeshaji maarufu nchini Kenya, Eric Omondi amewajia juu baadhi ya watu wanaoendelea kumkosa baada kuweka picha akiwa utupu katika mtandao wa kijamii licha ya kuomba radhi.

Kupitia ukurasa wake Instagram mchekeshaji huyo amesema hayo baada ya kushambuliwa kwa maneno makali na mashabiki zake na kutaka apelekwe Mahakamani ili aweze kujibu mashtaka ya udhalilishaji kutokana na kuweka mtandaoni video hiyo.

 Ameanza kwa kuandika “Sasa hivi kila kituo cha redio, ‘blogger’ pamoja na magazeti wanataka stori yangu, macho yao yote yapo kwangu, wanataka ‘attention’ yangu. Labda ni muda muafaka kwangu mimi kusema kuzungumza, kwasababu kuna mtu anaweza akasoma hichi nilichoandika na ninasali watu sahihi wasome”.

 Pia ameandika “Vipaumbele vyetu kama taifa vinaweza kuwa havijakaa sawa. Wakati tunajadili kuhusiana na kijana wa kiafrika ambaye aliogelea mtoni, kijana mdogo wa chuo alipigwa risasi na kufariki  na hospitali ya taifa ikamfanyia upasuaji mgonjwa mwingine asiyehusika. Ninatamani kujua stori ya kijana huyo. Alikuwa anasomea nini? ndoto zake ni zipi? alikuwa ni mtoto wa pekee”,.

Pamoja na hayo, Eric Omondi ameendelea kwa kusema “ninataka kuongea na kila mvulana na msichana, kila ndoto inaweza kutimia kuwa kweli. Kama unataka kuruka usikubali mtu mwingine akuambie huwezi au kukatisha tamaa, hata kama ni kuna nguvu ya mvutano ruka. Ila unatakiwa kuwa tayari kupanda milima na kushuka kwenye mabonde lakini mwisho wa siku utafika kileleni”.

Kwa upande mwingine, mchekeshaji huyo amewatia moyo vijana wenzake waendelee kupambana na huku wakumbuke kumtanguliza Mungu mbele ili wafike wanapopahitaji.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *