Muigizaji wa Bongo Movie, Wastara Juma amesema kuwa baada ya kufanyiwa vipimo vyote nchini India amebainika kuwa na tatizo kwenye fuvu lake la kichwa.
Wastara amesema hayo baada ya kuwasili nchini akitokea nchini India ambako alienda kufanyiwa matibabu ya mguu pamoja na mgongo.
Wastara ameendelea kwa kusema “nimefanikiwa kupata dawa pia na ninatakiwa nitumie kila baada ya miezi mitatu na kama kuna uwezekano wa kupata matibabu hapa hapa nchini itakuwa vizuri. Wenyewe wamenishauri kama itawezekana niweze kupata bima ya afya kubwa kwa sababu kama kuna ulazima wa kurudi kila baada ya miezi mitatu iwe rahisi ili niweze kuangalia tatizo la kichwa kwa sababu sio jambo la kulifanyia masihara”.
Kwa upande mwingine, Wastara amesema anamshukuru Mwenyezi Mungu kwa kumuwezesha kurudi salama nchini pamoja na tatizo lake la mguu linaendelea vizuri japokuwa bado yupo kwenye uangalizi.