Mwanamuziki wa hip hop nchini, Roma Mkatoliki amefungiwa na wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo kutojihusisha na muziki kwa miezi sita kutokana na nyimbo zake kukosa maadili.

Adhabu hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa wizara hiyo, Juliana Shonza baada ya kujiridhisha na makossa ya msanii huyo kutokana na nyimbo zake kukosa maadili katika jamii.

Naibu waziri Shonza amesema kuwa Roma amefungiwa kutojihusisha na shughuli zozote za muziki baada ya kukaidi agizo la kubadilisha mashairi ya wimbo wake wa Kibamia.

Pia Naibu waziri huyo amesema kuwa Roma amedharau agizo la serikali wa kubadili mashairi ya wimbo huo aliofanya na Stamina.

Kwa upande mwingine Naibu waziri Shonza amesema kuwa adhabu hiyo itajumuisha na nyimbo zake zote kutokupigwa Redioni wala kwenye runinga kwa muda wote aliyofungiwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *