Mahakama ya mwanzo wilaya ya Kinondoni imemtaka mwanamuziki wa Bongo Fleva, Shilole kulipa faini ya shilingi milioni 14 baada kupatikana na hatia ya utapeli.

Mwanamuziki huyo amepatikana na hatia ya utapeli na kusababisha hasara kwa kushindwa kufika katika shoo ya muziki iliyoandaliwa na Mary Mussa mwaka jana.

Mahakama ilibainisha kuwa Shilole alilipwa kiasi cha Tsh. Milioni tatu na  Mary Musa kwa ajili ya kutumbuiza siku ya mkesha wa Pasaka 2017 katika Ukumbi wa Heineken uliopo Mbagala-Kijichi jijini Dar es Salaam.

Hakimu wa mahakama ya Mwanzo Kinondoni, A. P. Mshingwa amesema Shilole amekuwa akitumiwa wito mara kwa mara na mahakama afike kusikiliza kesi yake lakini amekuwa akikaidi kufanya hivyo.

 

Baada ya hukumu hiyo Mahakama imemuamuru Shilole azilipe pesa hizo haraka ndani ya wiki moja vinginevyo mali zake zitaanza kukamatwa kwa ajili ya kulipa deni hilo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *