Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Shilole amesema kuwa baada ya kuingia kwenye ndoa miezi kadhaa iliyopita kwa sasa yeye na mumewe, Ashraf Uchebe wako kwenye harakati za kusaka mtoto.

Shilole amesema kama kawaida ya watu wengi huwa wanatarajia tu baada ya ndoa waone matunda ambayo ni mtoto, yeye na mumewe wako kwenye kutafuta mtoto na Mungu akimjalia atapata.

Mwanamuziki huyo amesema kuwa suala la mtoto kwasasa ndiyo walilolipa kipaumbele baada ya kufunga ndoa.

Shilole na Uchebe walifunga ndoa mwaka jana na sherehe yao kufanyika mwaka huu ambapo sasa ni mke na mume.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *