Taasisi ya Mo Dewji imetangaza orodha ya wanafunzi 22 wa elimu ya juu waliopata ufadhili kutoka katika taasisi hiyo kwa mwaka wa masomo 2017/2018 kupitia mpango wa Mo Scholars.

Wanafunzi hao ni Neema Charles, Winfrida Mrope, Henritha Rwegasira, Monica Ubushimbali, Suzana Mkindi, Hamisa Selemani, Beatrice Shupa, Phoebe Mwankemwa, Amon Abraham, Venance Makambe na Amos Ntandu.

Wengine ni Benjamin Mkondya, Ally Mashaka, Amuniri Sebarua, Iddi Mbilinyi, Samwel Ponda, Eram Temu, Busumilo Tumaini, Cosmadeus Mayunga, Amos Kashinje, Kelvin Ernest na Barnaba Barnaba ambao wote ni wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).

Akizungumza kuhusu ufadhili huo, Mwanzilishi wa Taasisi ya Mo Dewji, Mohammed Dewji aliwapongeza washindi kwa kufanikiwa kupata ufadhili huo, lakini akiwataka kujituma ili waweze kufikia malengo waliyojiwekea katika maisha yao.

Aliongeza kuwa, dhamira yake ni kuona Watanzania wengi wananufaika na mpango huo na amejipanga kuhakikisha kuwa idadi ya wanufaika wa mpango wa ufadhili unaotolewa na taasisi yake unaongezeka kila mwaka.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *