Mfalme wa Saudi Arabia, King Salman amefanya mabadiliko katika jeshi la nchi hiyo ikiwa ni pamoja na kuwafuta kazi Makamanda wa Vyeo vya juu jeshini akiwemo Mkuu wa majeshi.
Taarifa hiyo imetolewa na shirika rasmi la habari la Saudi Arabia la SPA ambapo limeeleza kuwa Mfalme Salman pia amefanya mabadiliko kwa Makamanda wa vikosi vya nchi kavu na vile vya angani.
Hadi sasa hakuna sababu yoyote ya mabadiliko hayo iliyowekwa wazi lakini inasemekana mabadiliko hayo kiasi flani yameshawishiwa na Mrithi wa Mfalme Mohammed bin Salman.
Mabadiliko hayo yataanza mara moja kutekelezwa baada ya mfalme kutongaza taarifa hiyo ya mabadiliko ya kijeshi.