Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Alikiba anatarajia kufunga ndoa siku ya Ijumaa na mwanamke wake wa siku nyingi kutoka Mombasa nchini Kenya.
Msanii huyo ametajwa kutaka kufunga ndoa na mrembo huyo aliyefahamika kwa jina la Amina Ijumaa ya wiki hii.
Taarifa hizo ziliaza kusambaa baada ya Abdu Kiba kueleza wiki iliyopita wakati akifanya mahojiano nchini Kenya.
Hata hivyo inafahamika kuwa Alikiba amekuwa akienda mara kwa mara Mombasa kutokana na kuwa na ukaribu na Gavana wa mji huko, Joho.