Wasanii wa muziki wa Bongo Fleva, Nikki wa Pili, Roma Mkatoliki, Rama Dee na Izzo Bizness wameonesha kuguswa na hukumu ya kifungo cha miezi mitano jela kwa mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi ‘Sugu’.

Kupitia akaunti zao za mitandao ya kijamii wasanii hao wameandika maneno tofauti kufuatia hukumu hiyo ya Sugu na mwenzake Emmanuel Masonga.

Wasanii hao wameoneka wakimtia moyo kuwa gerezani siyo kaburini hivyo atamaliza muda wake na kurudi uraiani kuwapigania wananchi wa Mbeya.

Nikki ameanza kwa kuandika “Nguvu ya Mungu ikapate kuwa nawe pamoja na familia yako, gerezani sio kaburini ‘stay strong’ Jongwe”.

Kwa upande wake msanii Rama Dee yeye amesema kuwa ameumizwa sana na bahari ya Sugu kufungwa jela miezi mitano na kudai si picha nzuri katika nchi yetu kwa mambo kama haya.

“Nasikitika sana kwa hii habari kama msanii pia kama rafiki wa Sugu, hii si picha nzuri”.

Naye Izzo Bizness ambaye anaiwakilisha Mbeya vizuri katika muziki wa Hip hop pia ameonyesha hisia zake na kumtaka Mbunge huyo kuwa mvumilivu na kusimama imara katika kipindi hiki.

Pia Roma Mkatoliki alikuwa na haya ya kusema juu ya kifungo cha Sugu “Hata hili lipatita’ stay strong Joseph Zaburi 35: 1-28 “.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *