Msanii wa muziki wa injili, Rose Muhando anatarajiwa kuwepo kwenye tamasha la Pasaka lililopangwa kufanyika Aprili Mosi kwenye Uwanja wa CCM Kirumba mkoani Mwanza.

Msanii huyo ambaye aliteka nyoyo za waamini wengi alipotea miaka ya hivi karibuni baada ya kukumbwa na misukosuko ikiwemo kashfa mbalimbali za utapeli, mbali na kuzindua albamu yake atapamba tamasha hilo ambalo linawahusisha wasanii mbalimbali wa muziki wa injili kutoka ndani na nje ya Tanzania.

Mkurugenzi wa Msama Promosheni ambaye ndiye muandaaji wa tamasha hilo, Alex Msama alisema:

 “Pia kulikuwa na kesi nyingi sana polisi zilikuwa zikimhusu, lakini kwa sasa amerudi tena kundini, alianguka kwa sasa amesimama tena, mashabiki wake wampokee ili aendelee kuwaburudisha mashabiki wake.

“Natumaini hii ni habari njema kwa mashabiki wa injili kwa sababu nyimbo za Rose Muhando zimekuwa zinapendwa na kuchezwa na watu wa kila rika na kila dini kutokana na uzuri wake,” alisema Msama.

Pia Msama alisema kuwa tamasha la mwaka huu kuna utofauti wa eneo la tukio kwa ajili ya Tamasha la Pasaka lakini ubora wa tamasha ni uleule na burudani ni ileile. Aprili 2 tamasha hilo la Pasaka litafanyika tena kwenye uwanja wa Halmashauri mjini Bariadi mkoani Simiyu.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *