Muigizaji wa Bongo Movie, Wema Sepetu amefunguka na kusema kuwa amejisikia vizuri na furaha baada ya kurudi kwa mara nyingine katika mitandao ya kijamii.

Furaha hiyo ya Wema  Sepetu inakuja kufuatia kurudi kwa akaunti yake ya Instagram ambayo ilidukuliwa na watu wasiojulikana na kuanza kuposti vitu tofauti na mwenye akaunti hiyo ambaye ni Wema Sepetu.

Wema Sepetu alikosekana mtandaoni takribani kwa mwezi mmoja kutokana na kudukuliwa kwa akaunti yake hiyo.

Kupitia akaunti yake hiyo ya Instagram ameandika “Namshukuru sana Tizzo, daah nime-miss kweli ukurasa wangu. Najua jinsi mlivyoni-miss kwa sana. ‘But it feels good to be back”.

Wapenzi na mashabiki wa Wema Sepetu wamepokea ujumbe huo kwa shauku kubwa huku wengine wakimpa maneno yenye faraja kutoka na kupotea mitandaoni kwa kipindi kirefu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *