Muigizaji wa Bollywood, Sridevi Kapoor amefariki dunia kutokana na mshtuko wa moyo akiwa na miaka 54.

Taarifa iliyotolewa na familia yake imesema Sridevi alikuwa na familia yake mjini Dubai kuhudhuria harusi wa mpwa wake.

Sridevi amekuwa kwenye tasnia ya filamu kwa miongo minne ambapo amefanikiwa kushiriki kwenye filamu 300 na baadhi ya filamu zilizompa umaarufu ni kama Mr. India, Chandni, ChaalBaaz na Sadma.

Sridevi alitajwa kuwa mmoja wa wasanii wachache wa kike waliopata mafanikio makubwa bila ya msaada wa wanaume.

Baada ya taarifa hizo, maelfu ya watu walikusanyika nje ya nyumba yake jijini Mumbai kwa ajili ya kutoa pole kwa msiba huo.

Kifo cha  Sridevi kinakuja ikiwa ni miezi miwili imepita tangu mjomba wake ambaye alikuwa ni moja ya waigizaji nguli wa filamu nchini humo, Shashi Kapoor aage dunia.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *