Jeshi la Polisi kupitia Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Muliro Jumanne limethibitisha kuwashikilia watuhumiwa watatu wenye majeraha ya risasi katika Kituo cha Polisi Oysterbay jijini Dar es Salaam.
Muliro amesema watuhumiwa hao ni wale waliokamatwa kwenye maandamano ya CHADEMA yaliyofanyika Februari 16 mwaka huu na kusababisha kifo cha mwanafunzi Akwilina Akwilini.
Pia kamanda huyo amekanusha taarifa ya kwamba majeruhi hayo hawajapatiwa matibabu tangu wakamatwe, amesema wote wamepelekwa katika hospitali za serikali hivyo hakuna asiyepatiwa matibabu kama inavyoelezwa.