Naibu Waziri wa Mambo ya ndani, Hamad Masauni ametangaza kwamba kuanzia tarehe 1 Machi mwaka huu kutakuwa na ukaguzi wa magari binafsi nchi nzima na kwamba kila gari litalipia stika ya ukaguzi ambayo gharama yake ni Shilingi elfu tatu.

Masauni amesema kwamba Wamiliki wa magari madogo wanatakiwa kupeleka magari yao katika vituo vya polisi ili yafanyiwe Ukaguzi kama yanastahili kuendelea kuwepo barabarani.

Pia Masauni aliongeza kwamba ‘Nataka madereva  wa pikipiki ambazo zitakamatwa na kukutwa zimesajiliwa kwa majina ya kampuni badala ya majina binafsi wachukuliwe hatua mara moja’.

Kwa upande wake Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani Tanzania, Fortunatus Musilimu alisema katika Ukaguzi wa magari madogo utakaoanza mwezi ujao, mtu atakaekiuka na kukataa kupeleka gari lake kufanyiwa ukaguzi atakamatwa na sheria itachukua mkondo wake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *