Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe jana usiku amekamatwa na jeshi la Polisi mkoani Morogoro kwa kosa la kuwatembelea madiwani wa chama cha ACT Wazalendo katika kata zao.
Zitto Kabwe wanamtuhumu kwa kufanya ziara ya chama cha ACT Wazalendo kutembelea madiwani wao katika kata mbalimbali kwenye mikoa 8 nchini.
Kutokana na maelezo ya Wakili wake, Zitto ametuhumiwa kufanya Unlawful Assembly S. 74 cap 16 ya Sheria ya Kanuni ya Adhabu.
Jeshi la Polisi limekataa kumpa dhamana na kumpeleka mahabusu ya Kituo Kikuu cha Polisi cha Mkoa wa Morogoro.
Wakili Mvula amesema pia Jeshi la Polisi limekataa kusema kama dhamana ipo wazi au la, au kuweka wazi masharti ya dhamana.