Vilio vimetawala wakati wa kuuga mwili wa mwanafunzi wa Chuo, Akwilina Akwiline aliyepigwa risasi na Polisi wiki iliyopita.
Mwili wa marehemu ulichukuliwa kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kuelekea katika viwanja vya chuo cha NIT kwa ajili ya kuagwa.
Jeneza lenye mwili wa mwanafunzi lilikuwa katika gari maalumu la kubebea maiti ambapo wakazi wa Dar es Salaam walipata nafasi ya kuuga.
Baada ya kuaga mwili wa mwanafunzi huyo, saa 10 jioni safari kuelekea wilayani Rombo mkoani Kilimanjaro kwa mazishi ikaanza na mazishi yatafanyika kesho.