Jeshi la Polisi nchini limetakiwa kuzingatia maadili ya kazi na kuacha kuwabambikia watu kesi ikiwa ni pamoja na kujiingiza katika vitendo vya rushwa.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Simon Sirro akiwa katika ziara yake ya kazi Mkoani Tanga na kusema kuwa askari atakayebainika kupokea rushwa na kuwabambikia watu kesi atachukuliwa hatua za nidhamu.

Amesema kuwa “Ninatembelea vituo vya polisi kukagua majalada ya kesi, kuangalia sababu za kesi kuchelewa. Pia, ninaangalia kama kuna kesi ambazo wahusika wamebambikiwa ili kuyafanyia kazi mambo haya,”.

IGP Sirro amesema endapo kama itabainika kama kuna watu wamebambikiwa kesi basi huyo askari aliyefanya hivyo atawajibishwa kulingana na sheria.

IGP Sirro yupo mkoani Tanga kwa ziara maalumu kwa ajili ya kukagua maendeleo ya jeshi la polisi nchini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *