Aliyekuwa mfanyakazi wa CRDB, Gura amehukumiwa kwenda jela miaka 93 baada ya kumkuta na hatia ya makosa 29 ya kughushi na mawili ya wizi wa Sh. milioni 29.8 za benki hiyo.
Aidha, mahakama hiyo imemtia hatiani Gura kwa kosa la kutakatisha Sh. milioni 29.8 na kumwadhibu kulipa faini ya Sh. milioni 100.
Mahakama imesema akishindwa kulipa faini hiyo atakwenda jela kutumikia kifungo cha miaka mitano na imeamuru arejeshe fedha hizo kwa benki hiyo, na akishindwa kitatolewa kibali cha kifilisiwa mali zake.
Hakimu Simba alisema mahakama yake imemtia hatiani kwa makosa 32 na kwamba kwa kosa la pili hadi la 30 mshtakiwa atakwenda jela kutumikia kifungo cha miaka mitatu kwa kila kosa.
Pia, alisema Hakimu Simba, mshtakiwa atatumikia kifungo cha miaka mitatu kwa kosa la 31 na 32 ya wizi wa Sh. 29,889,191 mali ya benki ya CRDB.
Gura alidai kuwa amekaa mahabusu kwa miaka mitatu, ni mwenye familia ya mke na watoto watatu wote wadogo na wenye kumtegemea.
Hakimu Simba alisema adhabu hizo za kifungo jela zitakwenda sambamba na kwamba mahakama imezingatia maombi ya mshtakiwa.