Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amesema kuwa Serikali imedhamiria kuboresha huduma za afya nchini.
Makamu wa Rais leo amefungua Jengo la Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Itilima lenye vyumba 43 vya kufanyia kazi.
Makamu wa Rais aliweka jiwe la msingi la ufunguzi wa jengo la upasuaji lililopewa jina lake Samia Suluhu Hassan katika hospitali ya wilaya ya Maswa.
Makamu wa Rais pia alipata fursa ya kuwahutubia wananchi kwenye uwanja wa Nguzo Nane wilayani Maswa ambapo aliwahakikishia wakulima wa pamba dawa za Viua Dudu zitapatikana kwa wingi na mapema kuanzia sasa na kati ya mwisho wa mwezi huu au mwanzoni mwa mwezi ujao.
Wakati huo huo Makamu wa Rais alipokea hundi ya shilingi 178,448,00 kutoka kwa Balozi wa China kwa ajili ya ujenzi wa bweni la wasichana wa shule ya sekondari ya Nkoma iliyopo wilaya ya Itilima pamoja na Vyerehani 50 kwa ajili ya Halmashauri ya Mji Bariadi.
Balozi wa China alimueleza Makamu wa Rais “ Simiyu ni mkoa unaokuja kwa kasi kwa maendeleo na Mkuu wa Mkoa na Viongozi wenzake wameonekana na nia ya kuleta maendeleo hivyo hatuna budi kusaidiana nao na kusaidia nia njema ya Rais Magufuli ya kuinua elimu na kujenga Tanzania ya Viwanda.”