Rais wa Marekani, Donald Trump amesema kwamba kuwapatia walimu silaha kunaweza kuzuia mashambulio ya risasi katika shule kama lile lililowaua watu 17 wiki iliopita mjini Florida.

Rais huyo wa Republican pia aliunga mkono wito wa kuwakagua wanakotoka wanunuzi wa bunduki. Manusura wengine wakati huohuo waliwataka wa bunge wa Florida kuweka udhibiti wa bunduki.

Majimbo kadhaa ya Marekani tayari yanaruhusu bunduki ndani ya vyuo na taasisi za elimu kulingana na tovuti ya kujihami katika vyuo. Jimbo la Florida hatahivyo halifanyi hivyo.

Rais huyo wa Marekani alisikiliza malalamishi ya mabadiliko ya sheria za umiliki wa bunduki siku ya Jumatano kutoka kwa wanafunzi 40 , walimu na familia.

Baadhi ya wale waliohudhuria hafla hiyo ya saa moja waliunga mkono wazo la rais Trump kuwahami walimu.

Lakini Mark Barden ambaye mwanawe aliuawa katika shambulio la 2012 katika shule ya Sandy Hook Elementary School mjini Connecticut – anasema ongezeko la bunduki sio suluhu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *