Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amewasili nchini Uganda kwa ajili ya kuhudhuria mkutano wa 19.
Rais Magufuli amewasili nchini humo kwa ajili ya kuhudhuria mkutano wa wakuu wa nchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki utakao fanyika Ijumaa hii ya February 23 mjini Kampala.
Rais Magufuli aliondoka leo jijini Dar es Salaam ambapo alisindikizwa na mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.
Rais Magufuli amepokelewa katika uwanja wa kimataifa wa ndege wa Entebbe, na Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo, Sam Kutesa na kuelekea katika Ikulu ya Entebbe kwa ajili ya kufanya mazungumzo na Rais Yoweri Museveni.