Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Ben Pol amefunguka na kusema kuwa ametukanwa sana mtandaoni baada ya kupaka rangi ya kijani nywele zake.
Ben Pol amesema kuwa hakuvunjwa moyo na matusi hayo ya mtandao kwasababu hiyo ni staili mpya aliyoichagua mwenyewe.
Kupitia mitandao ya kijamii, baadhi ya mashabiki wake walikuwa wanamponda kwa kumwambia kuwa hajapendeza baada ya kuweka rangi ya kijani kwenye nywele zake bora angebaki kama zamani.
Ben Pol amesema watu wanaongea sana kuhusu nywele zake na kuifanya kuwa ishu kubwa wakihisi labda kuna kitu nyuma ya pazia kinakuja.
Baada ya Ben Pol kuweka hivyo baadhi ya wanamuziki wengine nao wameonekana wakibadili muonekano wa nywele zao kama vile Alikiba aliyeweka rangi nyekundu kichwani, Ommy Dimpoz aliyeweka rangi ya njano kichwani.