Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prefesa Makame Mbarawa ametoa onyo kwa wakazi wa Mkoa wa Tabora wanaoendeleza ujenzi na kilimo kwenye hifadhi ya barabara.
Profesa Mbarawa amewataka wananchi hao kuacha mara moja shughuli hizo kwasababu serikali imetumia fedha nyingi kulipa fidia ili kupisha ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami.
Pia Prof. Mbarawa amesema serikali inatumia zaidi ya shilingi bilioni 894 kutekelza miradi mikubwa minne ya barabara wa kiwango cha lami zenye urefu wa zaidi ya kilomita 500 Mkoani Tabora.
Kwa upande mwingine, Waziri huyo wa Ujenzi amesema wakazi wote ambao watakua wameingia katika maeneo ya barabara hawatalipwa fidia yoyote.
Waziri Mbarawa amewataka wananchi hao waondoke haraka huku akisema serikali haitasita kuwalipa wale wote watakaopisha ujenzi wa barabara kwa mujibu wa sheria.