Waziri Mkuu wa Ethiopia, Hailemariam Desalegn amejiuzulu wadhifa huo baada kuandika barua kwa chama chake cha Ethiopia People’s Demecratic Front akiomba kuachia ngazi.
Desalegn amesema kuwa amejiuzulu ili kusaidia kusuluhisha mzozo wa kisiasa uliopo nchini humo.
Wananchi, wakeleketwa wa Ethiopia Peoples Revolutionary Democratic Front na serikali inataka kupata ufanisi wa mabadiliko yaliowekwa katika wakati ambapo kuna mgogoro na matatizo ya kisiasa nchini humo.
Wengi wamepoteza maisha, wengine makao huku mali zao zikiharibiwa na kuna juhudi za kuharibu uwekezaji uliopo.