Mzazi mwenza na mwanamuziki wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz, Zari the Boss Lady ametangaza kuvunja rasmi mahusiano yake ya kimapenzi na mwanamuziki huyo.

Zari amefunguka hayo kupitia akaunti yake ya Instagram ambapo amechukua uamuzi huo kutokana na Diamond kutokuwa mwaminifu kwenye mahusiano yao huku akibainisha kuwa kuachana katika mahusiano ya kimapenzi hakutaathiri uhusiano wao kama wazazi.

 Diamond alianza mahusiano na Zari takribani miaka mitano iliyopita baada ya kuachana na muigizaji wa Bongo Movies, Wema Sepetu.

 Diamond amezaa na Zari watoto wawili ambao ni Tiffah na Nilan ambao wanaishi na mama yao nchini Afrika Kusini.

Sababu nyingine iliyosababisha Zari kuachana na Diamond baada ya kuhusishwa kurudiana na Wema Sepetu.

Bado haijathibitika moja kwa moja iwapo kweli wameachana ama ni kiki kama ambavyo wasanii wengine wamekuwa wakifanya ili kukuza kazi zao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *