Muigizaji wa Afrika Kusini aliyejipatia umaarufu kupitia filamu ya Sarafina ‘Lalete Khumalo’ amefunguka kusumbuliwa na ugonjwa wa Vitiligo.
Katika maisha yake baada ya kuwa maarufu alipitia changamoto nyingi kama kuolewa na mwanaume ambaye alikuwa akimtesa.
Mwaka 2016 star huyo aliamua kuweka wazi juu ya ugonjwa unaomsumbua, ambao unaathiri kiasi kikubwa cha ngozi yake,unaojulikana kama ‘Vitiligo’.
Moja ya chombo cha habari cha Afrika Kusini kilimnukuu akisema kuwa “imechukua muonekano wangu lakini niko sawa, sitaki maisha yangu yawe kuhusiana na hali niliyonayo, kwani bado mimi ni yule yule muigizaji, mama na mke”.
Akisimulia zaidi kuhusu hali hiyo, leleti amesema alijigundua akiwa na miaka 24, mwanzoni alikuwa na hofu huenda mume wake angeacha kumpenda lakini baadaye alijikubali, na kuamua kufurahia maisha yake.