Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro amesema kuwa bado jeshi hilo inakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo ucheleweshaji wa upelelezi, rushwa pamoja na uwepo wa viashiria vya kihalifu.
IGP Sirro ameyasema hayo jana mara baada yakumuapisha Kamishina wa Polisi Zanzibar, Mohammed Hassan makao makuu ya jeshi la polisi Jijini Dar es Salaam zoezi ambalo amelifanya kwa niaba ya Rais Dkt.John Pombe Magufuli.
Kamanda Sirro amesema kuwa kazi ya polisi ni ya kujitolea na bado kazi hiyo inakabiliwa na changamoto nyingi hivyo hakuna budi kufanya kazi kwa juhudi kukabiliana na vitendo hivyo vya kihalifu.
Baada ya kula kiapo Kamishina huyo wa Zanzibar, Mohammed Hassan akapewa neno kutoka kwa Katibu wa Sekretarieti ya Maadili ya Utumishi wa Umma, John Kaole kwa kuambiwa anatakiwa kurejesha shukrani kwa kufanya kazi kiuadilifu na kuzingatia maadili ya utumishi wa Umma.
Rais Magufuli alishawahi kumueleza IGP Sirro kuwa bado kuna changamoto kwenye jeshi hilo la polisi na kumtaka kuzifanyia kazi zaidi.