Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Ramadhani Kailima amesema kuwa maandalizi ya uchaguzi mdogo yanaendelea vizuri.

Kailima amesema Tume inafuatilia kwa karibu maandalizi ya uchaguzi huo utakaofanyika Jumamosi Februari 17,2018.

Katika taarifa ya NEC iliyotolewa jana Kailima amepongeza jitihada zinazofanywa na msimamizi wa uchaguzi  na wasaidizi wake katika kuhakikisha changamoto zinazojitokeza zinapatiwa ufumbuzi wa haraka.

Amewashauri wasimamizi wa uchaguzi kuendelea kukutana na wawakilishi wa vyama vya siasa kwa ajili ya kutoa taarifa katika kila hatua.

Kailima amesema Tume imejipanga kuanza kutoa vipindi vya elimu ya mpiga kura mfululizo hadi siku ya uchaguzi.

Amesema elimu itahusu mada kadhaa zikiwemo haki na wajibu wa mpiga kura, wakala wa vyama vya siasa na msimamizi wa uchaguzi pamoja na taratibu zote za upigaji kura.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *