Muigizaji wa Mongo Movie, Wema Sepetu leo amepanda kizimbani katika mahakama ya hakimu mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam kusikiliza kesi yake inayomkabili ya matumizi ya dawa za kulevya.

Wema Sepetu amefika mahakami hapo akiwa ameambatana na wakili wake mpya katika kesi hiyo Alberto Msando baada ya wakili wake wa awali, Peter Kibatala kujitoa kumtetea muigizaji huyo.

Wema Sepetu akiwa mahakamani hapo leo
Wema Sepetu akiwa mahakamani hapo leo

Wema anakabiliwa na kesi ya kukutwa na msokoto wa bangi nyumbani kwake maeneo ya Ununio jijini Dar es Salaam mnamo mwaka jana wakati wa sakata la kukamata watumiaji wa madawa ya kulevya iliyoanzishwa na mkuu wa mkoa, Paul Makonda.

Kujitoa kwa Peter Kibatala kwenye kesi hiyo inasemakana ni baada ya Wema Sepetu kurudi CCM akitokea Chadema ambapo Kibatala ni mwanachama wa Chadema.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *