Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Vanessa Mdee amesema licha ya gharama kubwa ya kuandaa albamu yake mpya lakini yeye anachoangalia jinsi itakavyopokelewa na mashabiki.
Vanessa alizindua albamu yake hivi karibuni aliyoipa jina la ‘Money Monday’ katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam ambao amekiri kutumia milioni 100 kwa ajili ya kuandaa albamu hiyo.
Mwanamuziki huyo amesema kuwa hajutii kutumia kiasi hicho cha fedha kwa kuwa lengo lake kutoa kazi itakayoweza kumleta heshima ndani na nje ya Tanzania kutokana ubora wake wa kazi.
Pia Vanessa amesema kuwa anawashukuru mashabiki wake kuipokea vizuri albamu yake ya kwanza tangu aanze mziki.
Vanessa alikuwa nchini Nigeria kuitangaza albamu yake hiyo kwa ajili ya mashabiki wa nje ya Tanzania.