Jeshi la Polisi nchini Uganda limemkamata mtuhumiwa aliyehusika na kifo cha mwanamuziki maarufu nchini humo, Radio.
Mtuhumiwa anayejuliaka kwa jina la Wamala Godfrey mwenye umri wa miaka 28 ndiye alikuwa akisakwa na polisi kama mtuhumiwa mkuu mara baada ya mmiliki wa bar, Egesa George na Meneja wake kilipotokea kifo cha Radio kushikiliwa na Polisi.
Radio alifariki dunia Februari Mosi mwaka huu kutokana na majeraha ambayo aliyapata kichwani kufuatia ugomvi katika bar hiyo.
Kamanda wa Polisi Kampala, CP. Frank Mwesigwa amethibitisha kushikiliwa kwa Wamala Godfrey na kueleza kuwa kwa sasa wanaandaa majalada ili kuweza kumfikisha mahakamani.