Mwanamuziki wa Marekani, Rihanna amepingwa na vikundi vya dini nchini Senegal kuingia nchini humo.
Rihanna anategemewa kuhudhuria mkutano mkubwa nchini Senegal lakini vikundi vya dini nchini humo wamekataa kumpokea.
Shirika la vikundi 30 vya kidini wamemshutumu mwanamuziki huyo kwa kutumia ishara za mazo na kuwa mjumbe wa chimbuko la Illuminati lilanoaminika kuwa ni kundi maalum la watu ambao hudhibit masuala na uongozi wa dunia na inasadikika kuwa hufanya shughuli zao kisiri kudhibiti kila kitu na kuunda Utawala Mpya wa Dunia.
Rihanna atatembelea nchi hiyo ya Afrika Magharibi akiwa katika nyadhifa yake ya balozi wa shirika la elimu ‘Global Partnership Foundation’
Shirika hilo linamaadhui wa kuchangisha fedha za kuwafundishia mamilioni ya watoto na vijana katika nchi zinazoendelea.