Mwanasokka mkongwe wa Argentina, Diego Maradona amenyimwa VISA ya kuingia nchini Marekani baada ya kudaiwa kumtolea maneno ya Kashfa Rais wa nchi hiyo Donald Trump.
Maradona ambaye kwa sasa anainoa Klabu ya Al Fujairah ya Falme za Kiarabu alitarajiwa kusafiri kuelekea Miami kusikiliza kesi yake na mkewe wa zamani Claudia Villafane lakini maafisa usalama wamemnyima VISA.
Akiwa kwenye mahojiano siku za hivi karibuni Maradona alikaririwa akimuita Raisi Donald Trump ‘chirolita’ jina ambalo kwa nchi za Amerika ya Kusini wanalitafsiri kama Kikaragosi.
Kesi hiyo inayomkabili Maradona kwa sasa itasikilizwa na wakili wake na bado hadi sasa hakuna taarifa rasmi kama bado gwiji huyo wa soka duniani ataendelea kunyimwa VISA.