Muigizaji wa Bongo Movie, Wastara Juma leo anatarajia kuelekea nchini India kwa ajili ya matibabu ya mguu wake unaomsumbua.

Wastara amekamilisha kiasi cha shilingi milioni 37 alizokuwa akihitaji na leo anatarajia kuondoka nchini kuelekea kwenye Hospitali ya Sefaree iliyopo India kwa matibabu.

Wastara amesema kuwa hakutarajia muitikio mkubwa wa kuchangiwa fedha hizo na anawashukuru wote waliofanikisha kupatikana kwa msaada huo.

Muigizaji huyo amewashukuru watanzania kwa mchango wao waliompa mpaka kufanikisha safari hiyo ya kuelekea nchini India.

Wiki chache zilizopita muigizaji huyo alipokea milioni 15 kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na mkewe Mama Janneth Magufuli.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *