Mama watoto wa Diamond , Zarinah Hassan ameamua kuchukua uamuzi mgumu baada ya kum-unfollow mpenzi wake Diamond kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Hatua ya Zari imekuja kufuatia kusamba kwa video zikimuonesha Diamond akiwa na Wema Sepetu katika hafla ya utambulisho wa mwanamuziki, Mbosso.

Wengi walitegemea kuona Zari akimlushia vijembe baba watoto wake kama ambavyo imekuwa kipindi cha nyuma Diamond alipopata skendo na Hamissa  Mobeto.

Zari kupitia akaunti yake ya instagram yenye wafuasi milion 3 na zaidi ameamua kumu-unfollow baba watoto wake, Diamond Platinumz kitu ambacho kimezua gumzo mtandaoni.

”Hakuna siri katika maisha, unaweza kufikia malengo ikiwa una nia ya kuyafikia, na kufikia malengo yako unatakiwa kuamua na kuwa tayari”.

“Alituma post hiyo January 30, 2018, siku ambayo Diamond na Wema Sepetu wakiwa stori kubwa ya siku baada ya kuonekana klabu pamoja.

Hayo yamejiri siku chache zilizopita wakati wa uzinduzi wa kumtambulisha rasmi Maromboso katika familia ya WCB, Wema Sepetu akiwa kama mgeni mwalikwa katika shughuli hiyo.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *