Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Nay wa Mitego amesema kuwa wiki ijayo anatarajia kuachia ngoma yake mpya baada ya kukaa kimya kwa muda mrefu bila ya kuachia ngoma yoyote.

Nay ametoa taarifa hiyo kupitia akaunti yake ya Instagram na kuwataka mashabiki wake wakae mkao wa kula kwa ajili ya ngoma hiyo mpya inayotoka wiki ijayo kwa mujibu wa taarifa yake hiyo.

Pia kupitia ujumbe huo wa Instagram Nay wa Mitego amesema kuwa watu waliodukua akaunti zake na kufuta kazi zake toka aanze muziki anawajua ila hatolipa kisasi baada ya kumfanyia ubaya huo.

Nay ameanza kwa kuandika “Next Week ni Week Yetu, kuanzia Jumatatu Nitafungua Mwaka Boom Langu La kwanza Mwaka Huu.! Walihak Vitu Vyangu karibu vyote, Wamefuta kila kitu Changu Youtube Nawajua Wabaya Ila Sina Ubaya Nao”.

Ameongeza kwa kuandika “Sasa Ngoja Tuanze Mchaka Mchaka Nenda #Subscribe kwenye Youtube Chanel Yangu #MrNay Ili uwe wa kwanza  kuitazama na Kusikiliza Ngoma yangu Mpya Inayotoka Wiki Ijayo”.

Hiyo itakuwa ngoma ya kwanza kwa mwanamuziki huyo kwa mwaka huu baada ya kukaa kimya kwa muda mrefu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *