Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ametuma salamu za rambirambi kufuatia kifo cha mwanasiasa mkongwe nchini, Kingunge Kombare-Mwiru.

Rais Magufuli amesema kuwa amepokea kwa masikitizo na huzuni kifo cha mwanasiasa huyo mkongwe kilichotokea hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam.

Mzee Kingunge alilazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi (ICU) katika hospitali ya Taifa Muhimbili kufuatia kujeruhiwa vibaya na mbwa mpaka kupelekea kupata majeraha makubwa mwilini mwake.

Kifo cha mzee Kingune kimethibitisha na mwanawe, Kinjekitile Kingunge ambapo amesema kuwa baba yake amefariki dunia usiku wa kuamkia leo.

Mzee Kingunge atakumbukwa kwa kazi zake za siasa alizofanya toka akiwa ndani ya chama cha Tanu, CCM na hadi kuhamia upinzani kwenye uchaguzi wa mwaka 2015.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *