Watangazaji wa kipindi cha Shilawadu, Soudy Brown na Qwisah jana wamejikuta kaika wakati mgumu baada ya kupokea kichapo kutoka kwa dansa wa Diamond Platnumz, Mose Iyobo.
Ugomvi huo umetokea dukani kwa Aunty Ezekiel maeneo ya Kinondoni jijini Dar es Salaam ambapo watangazaji hao walifika dukani hapo kwa ajili ya mahojiano na Aunty Ezekiel kuhusu ugomvi wake na Tunda.
Siku chache zilizopita Aunty Ezekiel alianzisha malumbano na video vixen Bongo, Tunda baada ya Aunty kudai deni lake la pombe aina ya Belalie ambayo thamani yake ni shilingi laki moja.
Katika malumbano hayo, Tunda pia alimshirikisha Mose Iyopo kwa kumwita Kiben-ten kuwa alimpa ela ampe Aunty lakini akupeleka mpaka kupelekea Mose naye kumjibu Tunda kwa maneno makali.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram mtangazaji wa kipindi cha Shilawadu , Soudy Brown amesema kuwa wamepigwa na kuvunjiwa vifaa vyao mpaka kupelekea wenzao kuumia na kupelekwa hospitali kwa matibabu kufuatia kipigo hicho.
Shilawadu ni kipindi maarufu nchini kinachorushwa na Clouds Tv kila siku ya Ijumaa kuanzia saa tatu kamili, ni kipindi kinachoelezea masuala ya mbali mbali ya udaku yanayotokea kwa watu maarufu hususani wasanii wa Bongo.